Matokeo ya kidato cha nne 2023/2024. Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) leo January 25,2024 limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika November 2023 ambapo jumla ya Watahiniwa 484,823 sawa na 87.65% ya Watahiniwa waliofanya mtihani huo wamefaulu.
“Kati ya Wanafunzi hao waliofaulu kuna Watahiniwa wa Shule na Watahiniwa wa Kujitegemea ambapo jumla ya Watahiniwa wa Shule 471,427 kati ya 527,576 wenye matokeo ambao ni sawa na 89.36% wamefaulu ambapo wamepata madaraja ya I, II, III na IV, mwaka 2022 Watahiniwa waliofaulu walikuwa 456,975 sawa na 87.79% hivyo ufaulu
umeongezeka kwa 1.57%“
“Watahiniwa wa Kujitegemea waliofaulu mtihani ni 13,396 sawa na 52.44%, mwaka 2022 Watahiniwa wa kujitegemea 19,475 sawa na 68.34%!walifaulu mtihani huo. hivyo, faulu wa Watahiniwa hao wa kujitegemea umeshuka kwa 15.90% na mwaka 2022”
Social Plugin